|
Bukoba Kids ni Klabu ya michezo ambalo ni shirika lina madhumuni ya kuifanya Bukoba kuwa mahali pazuri kwa watoto na vijana ambao wanaweza kufurahia michezo wakati wakijifunza elimu ya afya, viungo na stadi za maendeleo ya jamii.
Kwa sasa Bukoba Kids ina misingi wa mtazamo wake ambao ni kuwa mojawapo ya Klabu ya michezo ya mpira wa miguu nchini Tanzania.
Kwa sasa tuna timu tatu za wavulana na moja ya wasichana ambazo tunajivunia.
Ingawa Bukoba Kids inathamani matokeo mazuri katika mazoezi, tunaamini kuwa kwa sasa nchi inayoendelea kama Tanzania michezo ni zaidi ya starehe au aina ya burudani.
Mwelekeo aliouonyesha katibu mkuu mstaafu wa umoja wa mataifa Kofi Annan alisema „watu katika kila nchi duniani hupenda michezo, umuhimu wa michezo ambao umwezesha mtu kuwa na nguvu na afya bora, vilevile uleta usawa ambao ni mafanikio kwa kila mtu. Inaweza kuwa ukombozi wenye nguvu wa maisha bora ya watu ambao wamekandamizwa na umaskini - hasa watoto“.
|